FUJO ZILIZOFANYIKA MJINI SUMBAWANGA SIKUKUU YA EID KATIKA PICHA!!! FFU na Police wako makini
 Hapa wakiwananakung'utwa mabomu tuu na kutimambio..


 Hapa disco la watoto linaendelea ndani police wanahakikisha nje kuna usalama wakutosha...
Jamani, kwakweli naomba tuu leo niwe muwazi nilikwazika sana na hichi kitendo...

Kama kawaida yangu chini ya TEDDY KAEGELE'S ENTERTAINMENT huwa napiga madisco sikukuu zote kuanzia eid, pasaka, christmas na mwaka mpya... sijawahi kuona fujo kama hizi hadi police ilibidi waingie kati... chanzo nasikitika kusema kulikua na baadhi ya waislam wa mkoa wa Rukwa hawakupendezeshwa na mimi nikiwa kama mkristo kupiga disco.

Jamani haina haja ya kugombana sisi wote ni binaadamu na kama mtu hupendi mwanao aje disco basi mwambie atulie nyumbani.. na nyie mlio leta fujo mnajijua na ninashukuru jeshi la polisi liliwashugulikia ipasavyo.... alafu mje kuchukua vibarakashee na yeboyebo zenu mlizoangusha wakati mnakimbia mabomu...
amani na upendo vitazidi kutawala mkoa wetu.

Comments