Wednesday, 10 April 2019

MFAHAMU TAHIYA SALUM MAARUFU KAMA SHANTALLE MMILIKI WA VIPODOZI VYA ASILI VYA SHANTALLE HERBAL PRODUCTS KUTOKA TANZANIA

Ni mwanzilishi wa SHANTALLE  HERBAL PRODUCT @shantalleproduct inayojishughulisha na uzalishaji wa vipodozi vya tiba na ngozi.
-
Haikuwa rahisi hata kidogo kufika hapo kwani alivyomaliza kidato cha 4 alisomea unesi na alivyohitimu hakuendelea na kazi, badala yake aliolewa. Changamoto za ndoa zilimfanya afanye biashara kwa kuibia kwani familia alipoolewa haikutaka ajishughulishe na chochote. Aliuza udi nyumba hadi nyumba kwa siri, madela na kukopesha. Watu walikopa na hawakuwa wakimlipa hivyo biashara ikafa na akaana kuuza chapati kupeleka maofisini akishirikiana na mfanyakazi wa pale nyumbani. Baadae yule mfanyakazi alikimbia na pesa zote na hakujua angempataje kwani ilikuwa ni siri.
-
AMEFIKAJE HAPO ALIPO?
-
Alianza kwa kutengeneza mafuta kwa watu ambao nywele zao zinakatika na wale ambao nywele zilipotea kichwani. Biashara rasmi alianza 2014 alivyoona matokeo mazuri kutokana na bidhaa yake, 2015 ndio alifungua rasmi kampuni na kuanza kwenda kwenye maonyesho akiwa na bidhaa moja ya mafuta ya nywele. Baadae akawa mzalishaji wa bidhaa zote za nywele yaani shampoo, steaming, hairfood, hairoil n.k
-
ALIANZAJE KUTENGENEZA MAFUTA MWANZONI?
-
Alisafiri kwenda India kumepeleka baba mkwe wake kimatibabu. Hivyo alifikia kwa wakwe zake maana walikuwa wana asili ya kihindi. Alichokuwa anakiona katika mazingira yale ni watu walikuwa wanaanika mbegu tofauti mara kwa mara.  Ilimpasa aulize, walimpa jibu kuwa ni dawa ya nywele. Alihamasika kujifunza zaidi kwa kutoroka na kwenda kujifunza na huko alipata fursa ya kukutana na mtaalam aliyekuwa akielekeza jinsi ya kuchanganya zile mbegu, aliulizia mpaka alipopata vipimo sahihi na aliviandika vyote.
-
Alirudi Tanzania na akapitia changamoto ya kutengana na mumewe, hivyo alirudi kwao akiwa hajui nini la kufanya. Siku 1 akiwa anatazama kumbukumbu ya picha ndipo alipoiona ile karatasi yenye maelekezo ya utengenezaji wa dawa ya nywele. Alizitafuta zile mbegu sokoni na kuanza kutengeneza dawa. Ilifanya vizuri kwa kila aliyekuwa anaitumia, na hapo ndipo alipoanza kuwekeza kibiashara zaidi. Alianza na mtaji wa Tsh 90,000  tu aliyopewa na mama yake.
-
2017 alipata tuzo ya malkia wa nguvu katika sekta ya retail.

#ukithubutuunaweza

No comments:

Post a Comment

MFAHAMU TAHIYA SALUM MAARUFU KAMA SHANTALLE MMILIKI WA VIPODOZI VYA ASILI VYA SHANTALLE HERBAL PRODUCTS KUTOKA TANZANIA

Ni mwanzilishi wa SHANTALLE  HERBAL PRODUCT @shantalleproduct inayojishughulisha na uzalishaji wa vipodozi vya tiba na ngozi. ...