Wednesday, 10 April 2019

MFAHAMU TAHIYA SALUM MAARUFU KAMA SHANTALLE MMILIKI WA VIPODOZI VYA ASILI VYA SHANTALLE HERBAL PRODUCTS KUTOKA TANZANIA

Ni mwanzilishi wa SHANTALLE  HERBAL PRODUCT @shantalleproduct inayojishughulisha na uzalishaji wa vipodozi vya tiba na ngozi.
-
Haikuwa rahisi hata kidogo kufika hapo kwani alivyomaliza kidato cha 4 alisomea unesi na alivyohitimu hakuendelea na kazi, badala yake aliolewa. Changamoto za ndoa zilimfanya afanye biashara kwa kuibia kwani familia alipoolewa haikutaka ajishughulishe na chochote. Aliuza udi nyumba hadi nyumba kwa siri, madela na kukopesha. Watu walikopa na hawakuwa wakimlipa hivyo biashara ikafa na akaana kuuza chapati kupeleka maofisini akishirikiana na mfanyakazi wa pale nyumbani. Baadae yule mfanyakazi alikimbia na pesa zote na hakujua angempataje kwani ilikuwa ni siri.
-
AMEFIKAJE HAPO ALIPO?
-
Alianza kwa kutengeneza mafuta kwa watu ambao nywele zao zinakatika na wale ambao nywele zilipotea kichwani. Biashara rasmi alianza 2014 alivyoona matokeo mazuri kutokana na bidhaa yake, 2015 ndio alifungua rasmi kampuni na kuanza kwenda kwenye maonyesho akiwa na bidhaa moja ya mafuta ya nywele. Baadae akawa mzalishaji wa bidhaa zote za nywele yaani shampoo, steaming, hairfood, hairoil n.k
-
ALIANZAJE KUTENGENEZA MAFUTA MWANZONI?
-
Alisafiri kwenda India kumepeleka baba mkwe wake kimatibabu. Hivyo alifikia kwa wakwe zake maana walikuwa wana asili ya kihindi. Alichokuwa anakiona katika mazingira yale ni watu walikuwa wanaanika mbegu tofauti mara kwa mara.  Ilimpasa aulize, walimpa jibu kuwa ni dawa ya nywele. Alihamasika kujifunza zaidi kwa kutoroka na kwenda kujifunza na huko alipata fursa ya kukutana na mtaalam aliyekuwa akielekeza jinsi ya kuchanganya zile mbegu, aliulizia mpaka alipopata vipimo sahihi na aliviandika vyote.
-
Alirudi Tanzania na akapitia changamoto ya kutengana na mumewe, hivyo alirudi kwao akiwa hajui nini la kufanya. Siku 1 akiwa anatazama kumbukumbu ya picha ndipo alipoiona ile karatasi yenye maelekezo ya utengenezaji wa dawa ya nywele. Alizitafuta zile mbegu sokoni na kuanza kutengeneza dawa. Ilifanya vizuri kwa kila aliyekuwa anaitumia, na hapo ndipo alipoanza kuwekeza kibiashara zaidi. Alianza na mtaji wa Tsh 90,000  tu aliyopewa na mama yake.
-
2017 alipata tuzo ya malkia wa nguvu katika sekta ya retail.

#ukithubutuunaweza

Saturday, 21 April 2018

FOMU ZA KUJIUNGA MISS RUKWA 2018


FOMU YA KUOMBA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MISS RUKWA 2018


SIFA ZA MSHIRIKI:

·         Awe na umri kuanzia miaka 18 mpaka 24
·         Awe raia wa Tanzania ambaye hajaolewa wala kuzaa
·         Awe na uwezo ufahamu wa kutosha kujieleza na hasiwe mwanafunzi wa shule ya msingi awe amemaliza sekondari (Form IV)
·         Asiwe ameshiriki mashindano yaliyochini ya Kamati ya Miss Tanzania mwaka 2018. (Maana yake hairuhusiwi kushiriki mara mbili katika mwaka mmoja)


Kwa Maelezo Zaidi Piga 0762200027 au 0658200027


R.I.P AGNES GERALD (MASOGANGE)TANZANIA'S FAMOUS VIDEO VIXEN AGNES GERALD FAMOUSLY KNOWN AS "AGNES MASOGANGE" PASSED ON 
ON 20TH APRIL 2018.
R.I.P AGNES GERALD
8/09/1989 - 20/04/2018
REST WITH THE ANGELS
YOU WILL BE MISSED A LOT!

Monday, 16 April 2018

MISS RUKWA 2018

MISS RUKWA 2018
Inaletwa kwenu na Teddy Kaegele Entertainment
Kwa mawasiliano jinsi ya kudhamini au kushiriki piga simu namba: +255 762 200027

MFAHAMU TAHIYA SALUM MAARUFU KAMA SHANTALLE MMILIKI WA VIPODOZI VYA ASILI VYA SHANTALLE HERBAL PRODUCTS KUTOKA TANZANIA

Ni mwanzilishi wa SHANTALLE  HERBAL PRODUCT @shantalleproduct inayojishughulisha na uzalishaji wa vipodozi vya tiba na ngozi. ...