KWA MUDA MREFU TUMEKUWA KATIKA HARAKATI NA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA TUNAWAHABARISHA, ELIMISHA NA KUJADILIANA NA WADAU MBALIMBALI WA BLOG HII BILA KUINGIA UHURU WA WENGINE WALA KUKOSOA WENGINE, KWANI MAENDELEO YA KWELI YANATOKANA NA KUJIAMINI.
KWA MANTIKI HII TUNAOWAMBA RADHI WADAU WETU KWA KUTOKUWEPO HEWANI KWA SAA KADHAA LAKINI SASA MO BLOG IMERUDI NA ITAENDELEA KUWALETEA HABARI NA BURUDANI MBALIMBALI NANYI MSISITE KUTUSHAURI NA KUTUONGOZA KWA MAWAZO YA KUJENGA.
IKIWA NI MARA KWA MARA TATIZO HILI LA KUPOTEA NA KUPOTEZA KAZI ZETU KUTOKEA KATIKA BLOG YETU ,TUNAJIULIZA NI WAPI TUNAKOSEA AU KUHARIBU KATIKA UHABARISHAJI WETU WA HABARI NA MATUKIO ,AU KUFANYA HIVI NI MAKOSA..?!!!
KWA KIFUPI MOBLOG INATEMBELEWA NA WATU 20,000 KWA SIKU NA HILI LINATUPA NGUVU NA KUFAHAMU KUWA WADAU WETU WANARIDHISHWA NA KUPENDEZWA NA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, BIASHARA, MICHEZO, BURUDANI NA INTERVIEWS ZA WATU MAARUFU WANAOJULIKANA NA WALE PIA WENYE VIPAJI WASIOJULIKANA.
WADAU HILI NI KOSA…???
KWA MASIKITIKO MAKUBWA TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA KAZI ZOTE ZA MWAKA HUU 2011 ZILIZOPENDWA NANYI WADAU NA NYINGINE ZIKITOKANA NA MCHANGO WA NINYI WADAU NA WASOMAJI ZIMEPOTEA KWA LUGHA NYINGINE (ZIMEFUTWA/ZIMEPOTEZWA) KWA SABABU AMBAZO ZINATUTIA SHAKA NA KUTUPA HISIA KUWA NI ZA KIPINZANI.
TUSINGEPENDA KUSEMA MENGI NA WALA KUTAJANA MAJINA ILI KWA WEMA KABISA NA HEKIMA TUNAPENDA KUSISITIZA KUWA UPINZANI WA KUHARIBIANA SI MZURI NA HAUJENGI WALA KULETA MAFANIKIO KWANI MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
HAIPENDEZI KUONGEA HAYA YOTE HAPA ILA YAKIZIDI NI AFUENI YA MOYO NI KUONGEA NA KUSEMA WAZI TUMECHOKA KUHUJUMIWA.
ASANTE KAKA MAKWAIYA KWA MSAADA WAKO, MKUBWA MICHUZI TUNAKUSHUKURU BILA KUMSAHAU MZEE WA FULL SHANGWE NA WENGINE KWA MISAADA MBALIMBALI NA USHAURI MLIOTUPA KWETU.
WADAU WA MOBLOG TUKO PAMOJA NATUTAENDELEA KULIJENGA TAIFA LETU KWA AMANI, UPENDO NA MATUMAINI.
TUNAWAPENDA, TUNAWATHAMINI, TUNAWAHESHIMU NA TUTAFANYA KAZI PAMOJA NA TUTAFIKA PALE TUNAPOKUSUDIA.
MUNGU IBARIKI MO BLOG NA WADAU WAKE WOTE.
Endelea kuperuzi MO BLOG www.mohammeddewji.com/blog