Monday 15 November 2010

MY LOTION BEAUTY TIPS...By TK (TEDDY KALONGA)



Hello! warembo, sasa ni wakati wa kupata ile ngozi yako nzuri asilia unayoi'wish kuwa nayo. Namaanisha kuwa na ngozi yenye afya na mwonekano safi kama haijawahi kuharibiwa na jua. 

Mara nyingi tumekuwa tukishirikiana pamoja kuzungumzia products ambazo tunazigundua kuwa ni nzuri baada ya kutumia. Kuna waliobarikiwa kuwa na ngozi nzuri na kuendelea kuwa kama ilivyo maisha yao yote, lakini kuna wengine ambao walizaliwa na ngozi nzuri baadae ikatokea kuharibiwa na jua, hali ya hewa, make-up au vitu tunavyopaka mwilini. Hivyo nakupelekea kuwa na "ups and down" katika ku'maintain ngozi zao wakati wakitafuta kinachowatenda vyema. Ndio pale unakuta mtu anaamua kujichubua, kama njia moja ya kutafuta ngozi nzuri nyororo, isiyo na magamba, chunusi au sugu, ingawa si jawabu la kupata ngozi bora unayoitaka.

Naamini kuwa mpaka mtu anafikia kujichubua ni uwamuzi wa mwisho kabisa ambao unachukuliwa pale mtu anapochoka kuwa na ngozi ambayo haridhiki nayo.

Swali linakuja, wote tunataka kitu kimoja,... - NGOZI BORA NA NZURI.
Nzuri kivipi?...- Nyororo, isiyokuwa na madoa au chunusi. Teke, isiyokuwa na rangi mbili(pepsi mirinda). Yenye afya, inayovutia na kukufanya ujisikie vizuri, mrembo. Kwa sababu urembo wa mwanamke uko kwenye ngozi, nywele, meno na kucha. Na mwanamke yeyote anayezingatia hivi anakuwa na sifa ya kuitwa mwanamke msafi. USAFI ni sehemu moja ya urembo!

Kama mmoja wa wahusika wa kupenda kuji'take'good care "kila sehemu" (kuilea vyema ngozi yangu), nimeweza kutengeneza Lotion ambayo imeonekana kuniridhisha moyo100%, kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kushare na wewe mrembo. Hii kutokana na baada ya kuwatumia wadada kutoka sehemu mbali mbali na wote kutokea kupendezwa nayo, "MyLotion".

MyLotion, ni lotion inayobeba vitu asilia vitakavyoweza kuipa ngozi yako mwonekano wa ngozi moja ikiwemo SPF 100+, vitamin E, C. Uondoa weusi wa shingo uliosababishwa na jua, sugu za miguu na mikono, utengeneza unyororo, na kuipa ngozi yako mwonekano mzuri asilia. It smells good too!:)...

LOVE TK.

1 comment:

  1. There's no such a thing as SPF 100+.

    ReplyDelete