TAARIFA YA MO BLOG KWA WADAU...

MO BLOG INAPENDA KUWAFAHAMISHA WADAU  NA WASOMAJI WA BLOG HII KUWA TUMESIKITISHWA NA KUHUZUNISHWA NA TABIA INAYOENDELEA YA KUHUJUMIWA NA WAPINZANI WASIOPENDA MAENDELEO YETU KWA SABABU ZAO BINAFSI.

KWA MUDA MREFU  TUMEKUWA KATIKA HARAKATI NA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA TUNAWAHABARISHA, ELIMISHA NA KUJADILIANA NA WADAU MBALIMBALI WA BLOG HII BILA KUINGIA UHURU WA WENGINE WALA KUKOSOA WENGINE, KWANI MAENDELEO YA KWELI YANATOKANA NA KUJIAMINI.

KWA MANTIKI HII TUNAOWAMBA RADHI WADAU WETU  KWA KUTOKUWEPO HEWANI KWA SAA KADHAA LAKINI SASA  MO BLOG IMERUDI NA ITAENDELEA KUWALETEA HABARI NA BURUDANI MBALIMBALI NANYI  MSISITE KUTUSHAURI NA KUTUONGOZA KWA MAWAZO YA KUJENGA.

IKIWA NI MARA  KWA MARA TATIZO HILI LA KUPOTEA NA KUPOTEZA KAZI ZETU KUTOKEA KATIKA BLOG YETU ,TUNAJIULIZA NI WAPI TUNAKOSEA AU KUHARIBU KATIKA UHABARISHAJI WETU WA HABARI NA MATUKIO ,AU KUFANYA HIVI NI MAKOSA..?!!!

 KWA  KIFUPI  MOBLOG  INATEMBELEWA NA WATU 20,000 KWA SIKU  NA HILI LINATUPA NGUVU NA KUFAHAMU KUWA  WADAU WETU WANARIDHISHWA NA KUPENDEZWA NA  HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, BIASHARA, MICHEZO, BURUDANI NA INTERVIEWS ZA WATU MAARUFU WANAOJULIKANA NA WALE PIA WENYE VIPAJI  WASIOJULIKANA.

WADAU HILI NI KOSA…???

KWA MASIKITIKO MAKUBWA TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA  KAZI ZOTE ZA MWAKA HUU 2011 ZILIZOPENDWA NANYI WADAU NA NYINGINE ZIKITOKANA  NA MCHANGO WA NINYI WADAU NA WASOMAJI  ZIMEPOTEA KWA LUGHA NYINGINE  (ZIMEFUTWA/ZIMEPOTEZWA) KWA SABABU AMBAZO ZINATUTIA SHAKA NA KUTUPA HISIA KUWA NI ZA  KIPINZANI.

TUSINGEPENDA KUSEMA MENGI NA WALA KUTAJANA MAJINA ILI KWA WEMA KABISA NA HEKIMA TUNAPENDA KUSISITIZA KUWA UPINZANI WA KUHARIBIANA SI MZURI NA HAUJENGI WALA KULETA MAFANIKIO KWANI MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

HAIPENDEZI KUONGEA HAYA YOTE HAPA ILA YAKIZIDI NI AFUENI YA MOYO NI KUONGEA NA KUSEMA WAZI TUMECHOKA KUHUJUMIWA.
 ASANTE KAKA MAKWAIYA KWA MSAADA WAKO, MKUBWA MICHUZI TUNAKUSHUKURU BILA KUMSAHAU MZEE WA FULL SHANGWE NA WENGINE KWA MISAADA MBALIMBALI NA USHAURI MLIOTUPA KWETU.

WADAU WA MOBLOG TUKO PAMOJA NATUTAENDELEA KULIJENGA TAIFA LETU KWA AMANI, UPENDO NA MATUMAINI.
TUNAWAPENDA, TUNAWATHAMINI, TUNAWAHESHIMU NA TUTAFANYA KAZI PAMOJA NA TUTAFIKA PALE TUNAPOKUSUDIA.

MUNGU IBARIKI MO BLOG NA WADAU WAKE WOTE.

Endelea kuperuzi MO BLOG www.mohammeddewji.com/blog

Comments

 1. Hey there! I know this is sort of off-topic but I had to ask.
  Does running a well-established website like yours take a lot of work?
  I am completely new to blogging but I do
  write in my journal on a daily basis. I'd like to start a blog so I can share my experience and feelings online. Please let me know if you have any suggestions or tips for new aspiring blog owners. Thankyou!

  my web site :: how can i buy instagram followers online
  Also see my web site > how to get a lot of followers on instagram

  ReplyDelete

Post a Comment